Search This Blog

Thursday, November 3, 2022

USHUHUDA WA KWELI NAMBA 96

    




 Tanga miaka ya 82. Kuna jama alifanya mapenzi na mke wa mtu. Ghafla alipomaliza kitu kikakatikia ndani lkn damu haimwagiki. Alikuja kwa mganga pale Gatundu. Mtu mwingine ukimuangalia mashine unaiona imetulia. Yeye binafsi haioni na hata akipeleka mkono anakuta hamna kitu.

...........,..................



Jamaa mwingine tena alitembea na mke wa mtu. Wakamaliza fresh kila mtu akachukua hamsini zake. Jamaa alikua anakakaa nyumba isiyo na ceiling board. Ghafla wakati amepumzika chumbani kwake ametulia kitandani baada ya kumshuhhulikia mke wa bwege akaona panya amebeba dhakari na pum*** anakatiza nayo kwenye mbao juu





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 95

    




 Vibwengo nishawahi kutana navyo nikitoka bar night kali yaani vifupi kwa mbali vikija unaona kama taa inakufuata vinawaka taa kwenye paji la uso halafu vifupi na vidole vya miguu ya mbele vimegeuka nyuma yaan namaanisha mguu na vidole vinaangalia nyuma kwa hyo vikitembea kwa mbele unaona visogo vya miguu



.ukitembea ukikutana navyo usigeuke nyuma sasa we jitie van dame geuka uone umenikumbusha mbali mzee




USHUHUDA WA KWELI NAMBA 94

    




 Nina chapter mbili (2), moja ya kwangu ma ya pili ni ya baba yangu,

Nitaanza na yangu mwenyewe..

Mwaka 2016 nikiwa na umri wa kati tu usio na tija kuwa mme wa mtu, ila kutokana na misukumo na vishawishi vya barehe ikanibidi nivute kibinti cha kiislam, kutokana na kuwa nilikuwa mpambanaji wazazi wake waliniamini na kunipa mtoto wao japo sikuwa na kigezo hata cha kuoa wakati ule (20+ yrs only) sasa basi baada kufanya process zote ilibidi niowe kiislam kutokana na kuwa waslam hawana mambo mengi(mimi sio muislam wala sina mpango wa kuwa), yaani wao hata mkiwa watu 10 ndoa inatamadadi na kukwishineyi...sasa wakati ule wa binti kuvundikwa baadhi ya wenyeji, dungu&jamaa walianza kumletea zawadi za hapa na pale, baadae ndoa ilifungwa na maisha ya ndoa yakaanza rasmi, sasa kimbembe kilianza baada ya yeye kutoka kwao tu, yaani binti yule akawa mgumu kutoa papuchi ilihali alinipenda mwanzo na alilia ndoa kwa udi na uvumba sasa nikawa najiuliza huyu vipi, ama ananiectia..basi kwa akili zangu za ujana ujana nikawa na-force game, kisha kibishi namaliza ila alikuwa analia sana kana kwamba alifosiwa kuolewa..

Baada ya zile siku saba za mwanzo baada ya ndoa (honey moon) huko kijijini kwetu, tukawa tumejisogeza maghetto kwangu ili tuyaanze maisha yetu wenyewe, sasa hapo ndipo picha lilianza yaani binti kuanzia asubuhi-saa12 mzima kabisa yaani yupo shwari kimbembe ni ile kigiza cha usoni kikianza kuingia yaani alikuwa mwehu kabisa, sasa nikaanza kujiuliza hii imekaaje ama ndio mke ana act ili asitoe mchezo, basi ikabidi nitoe taarifa ukweni maana hali ifikia pabaya sana,

Sasa wakawa wameniambia kuwa jambo hili linavinasaba vya kishirikina, kwa upande wangu sikuamini hata kidogo, sasa bibi wa mke wangu mzaa mama mkwe alikuwa ni mrokole kindakindaki, basi wakawa wame- organize mama&bibi ili mtoto wao atibiwe hayo maswaibu..basi bana siku hiyo nakumbuka niko zangu ghetto sina hamu hata kidogo na ile ndoa si mama mtu akaja na yule Bibi akiwa na wenzake na mama zake wadogo, mama mkwe na wadogo zake ilibidi wabaki nje kutokana na kulinda itifaki ya kutoingia chumba cha mkwilima wake,

Wakawa wametutaka siye wanandoa tupige magoti ili ombi lianze humo humo ghetto, mwanzoni me nilikuwa na- take easy tu nahisi kama vile movie za kibongo, lakini baada ya ombi kukolea nikamuona wife kaanza kupiga mwano, wakabidi wakomae nae me nipo nacheck tu (ilibidi nifumbue macho) ombi likawa ombi daaah mara mtu chini wapo nae tu, mara wakaanza kuyahoji majini baada ya yule binti kuanza kusema mtuache, mnatuchoma..sasa hapo me siamini tu baada ya kuzungumza nayo yakawa yamesema kuwa pindi binti yule anafundwa ndani siku zile za kuvumdikwa kuna mtu alimpea under wear (chupi) kupitia kwa mdogo wake, yeye pasina kujali akawa kaivaa, na ndipo yalianza maswaibu..me bado hapo sina imani tu na kile kinachoendelea, baadae kabisa baada ya ombi kukolea yule binti akaanza kutema nyama nyama kama stake hivi ila zipo mithiri ya damu iliyoganda, wakachukua mtandio wake wakaanza kumtoa zile nyama mdomoni pia alikuwa anatafuna meno kiasi kwamba unasisimuka kama mtu anae sugua sifuria, hapo sasa ndio nikaanza kupata imani kuwa kweli binti yule ana jambo tena kubwa tu, baada ya ombi kumchek yule binti mdomoni nilishangaa hakuwa na jeraha wala kovu ambalo lilisababisha kutoa nyama zile tena zimejaa kwenye mtandio wake wa kiislam..mzee nilidata mpaka nikakoma na kimbelembele changu cha kuyakimbilia mapenzi,

Baada ya ombi lile tukawa kama temeyaamsha, na siku zilizofuata ndio kikawa kimbembe zaidi ya mwanzo, maana kuna usemi unadai kuwa kama wewe umeombewa na kutokwa na majini basi unatakiwa uishike imani sana sana laasivyo huwa yakitoka 10 yanarudi 20 it means (2x2), sasa sisi tuka- take easy kabisa, yaani majanga yalizidi mpaka kufikia hatua ndoa kuota mbawa ndani ya mwezi mmoja tu(mpaka sasa nipo single, na sina hamu kabisa ya kuwa na mke).

Yaani yule binti alipoteaga, wazazi wake waliuza nyumba ili kumtafuta binti yao kwa wataalamu, walimpata baadaya ya mwaka mmoja (2017) ila waliyumba sana kiuchumi na kuhama mji waliokuwa wanaishi na kwenda kwingine kuanzisha maisha tena ya upangaji, baba mkwe wangu na baba yake mzazi mpaka leo hawasemshani maana ktk jopo lililohusika na hizo inshu pia mke mdogo wa huyu babu wa mke wangu alihusika sana, pia huyu babu hakuwahi kusimama kumtetea mjukuu wake wakati wote alisema kuwa mkewe anasingiziwa huenda ni kutokana na limbwata ama juju alilopewa na huyo mke wake



NB: pia kipindi tunamuuguza mke wangu tuliwahi kwenda kutibiwa kwa mmoja wa bibi zake wa ukoo tukiwa huko, me nyege zikanizidi ikabidi nimuombe show wife maana tulilala kitanda kimoja, alivyogoma kutoa mechi ikabidi nitumie force maana nilikuwa na kama wiki kadhaa pasipo kufanya chochote kwake na isitoshe kwa wakati huu alikuwa keshapona(hapandwi na majini wala hakuwa kichaa), yule bibi alituachia room ambayo ilikuwa ndio kilinge chake, Aiseee nakumbuka wakati na-force kuchojoa chupi nae hayumo kelele zikawa kibao wakati huo ni kama saa11 alfajiri, mara paaap nasikia sauti kwenye angle ya kuta ikisema shiiiiiiiiii, daah nilitoka nje nikiwa na boxer yangu tu hapo nipo kifua wazi nikamfuata yule bibi akaniambia nitulie tu nikiwa ndani maana kilingeni huwa hakuhitaji makelele, sikuomba match tena wala sikusinzia mpaka kunapambazuka kisha nikasepa zangu kurudi mjini..





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 93

    



 Mwaka 2006 nipo Depo mkoa fulani, tulikuwa na utaratibu makuruta kwenda lindo usiku, na zamu ilikuwa ni vyumba, sasa siku hiyo ilikuwa zamu yetu tukaenda lindo mimi na washikaji wawili ambao tulikuwa tunakaa room moja, tukamuacha mmoja analinda room yetu.

Lindo letu lilikuwa karibu mtoto mkubwa, tumefika pale mida ya saa nne ilipotimu saa 7 usiku mauzauza yakaanza wale washikaji wawili wakaanza kupiga kelele kuweweseka kama vile wanagombana na mtu, "hatuji huko, hatutaki" nikawauliza ni nini hawanijibu, baadae wakakimbia wakaniacha mwenyewe kwenye lindo, baadae walikuja na guard commander wakadai kuna mtu alikuwa amekaa katikati ya maji alikuwa anawaita na kuwavuta kwa nguvu.



Kesho yake tumelala chumbani mmoja wa vijana akakimbia akazima taa ya chumbani akatulazimisha wote tujifunike blanket kuna mgeni na akatoa tahadhari atakayechukungulia atakiona, baada ya dakika moja nilisikia kishindo chumbani kama mtu ameshuka toka darini, baada ya robo saa nikasikia yule kijana anaongea anamuaga mtu.

Asubuhi tumeamka kijana amechanjwa chale mwili mzima, nilipomuuliza akasema ndugu zake walikuwa wamekuja kumtenengezea dawa kutokana na masahibu ya jana yake, kijana alikuwa mtu wa Rukwa.



Story ya pili.

Tupo lindo usiku tena tulikuwa watatu tena (sio wale wa mtoni) sehemu tuliyokuwa lindo ni njia ambayo raia wa kawaida hupita wakienda makwao, sasa siku hiyo mida kama ya saa sita kuna njemba moja ilipita, vijana wakaruka nae, pigwa sana, akagaragazwa sana, mimi nilikuwa nimepitiwa na usingizi, niliposhtuka nikawakataza wale wenzangu tukamwaachia akaenda zake, baada ya nusu saa yakaanza mauzauza, walikuja bundi wawili wakatuzunguka, halafu wakaondoka ghafla wale wenzangu wakaanza kuchapwa fimbo, chapwa sana lakini hawakimbii wanalia wanaomba niwasaidie, ilibidi usiku huo tutafute wenyeji waende kuomba msamaha kwa ile njemba iliyogaragazwa.



 





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 92

    




 Hebu nisimulie hiki kisa changu...



Jumanne 23-08-2019.



Ilikuwa saa nne na nusu usiku nikiwa nimeketi sebuleni,mara gafula mzee akatoka chumbani na kuanza kunitukana matusi ya nguoni...

"Kijana gani wewe kazi kula na kujaza choo,huoni wenzio wanafanya kazi na wanategemewa na wazazi wao...ni bora ningezaa hata mbuzi ningefaidi mchuzi.."

Mara ghafula nashutuka kofi hili hapa sijakaa vizuri ngumi hii hapa,nikasimama imara na kumkazia tu macho...wadogo zangu na mama yangu wakitazama tu pasi na kusema neno.

Nikageuka taratibu na kutoka nje,chozi la uchungu likanitoka ilikuwa ni siku mbili tu toka nifukuzwe shule moja niliyokwenda kuomba ajira ya kujitolea..ati hawawezi kuajiri kiziwi!.

Nilitazama anga jeusi lililosheheni nyota nyingi,mwezi uliotoa nuru angavu nikajiuliza "Mungu upo wapi?".. Nikaingia chumbani na kuvaa viatu.. Nikatoka naenda wapi? Sijui!

Nikaambaa nisijue kama nakanyaga ardhi au ninapaa,napishana na mtu ama kisiki,ilinichukua nusu saa kuuacha mtaa wetu nikaingia mtaa wa pili,huu ulikuwa na watu wachache zaidi na nyumba zilikuwa mbalimbali kiasi.

Nikakatiza pembeni ya makaburi,nikasimama,nikayatazama na kujiuliza " kwanini nisingekuwa nimelala pale? Nipumzike!"...loooh lakini sauti nyingine ikaniambia "una uhakika ukilala pale utapumzika? Nikagutuka nikatazama huku na huko hakuna kiumbe nikaongoza njia kuliacha eneo la makaburi na kuzidi kupotelea mbali zaidi na nyumbani.



Hatimaye nikawasili sehemu pweke,barabara kubwa ya kokoto,kulia na kushoto kukiwa na msitu na vichaka vingi,kiza ni kingi kutupia macho simu yangu ni saa sita na robo usiku!

Ikafika mahali kuna njia panda na upande wa kulia kuna mti mkubwa sana aina ya mbuyu mahali pana pana joto sana bwana,pana joto kali,mapigo ya moyo yakanienda mbio " duuucha dunduncha ducha dunduncha" sasa mapigo niliyasikia hadi masikioni..

Nywele zikanisimama na vipele vya uoga vikanitoka hewa ikawa nzito na uvumilivu ukaniisha na sasa nikatimua mbio hata nilipoliacha eneo lile kwa umbali wa mita mia mbili hivi,na sasa nikaanza kutoka katika makazi ya watu.

Kufika hapa ikanipasa kujiuliza ni wapi naelekea,sikuwa napajua napoelekea kumbukumbu ya misukosuko ya kimaisha na masimango yasiyoisha zikanijia,woga wote ukabiisha donge zito la uchungu,hasira na kukata tamaa likanivaa,machozi yakanitoka,nikashika njia na kuendelea na safari,safari isiyojulikana!

Baada ya mwendo wa dakika ishirini hivi nikaingia katika barabara kubwa ya lami,nikashika uelekeo wa kushoto,ilielekea ufukweni,baada ya masaa mawili hatimaye nikawasili ufukweni,nikazitupia macho hoteli kadhaa zilizotamalaki eneo lile,nikaachana nazo na kushuka mchangani mbali kidogi na mahoteli yale,nikajikalisha kitako na kutafakari nilipotoka,nilupo na ninapoelekea,lakini mbona mbele kyna kiza kizito!





KIZAAZAA!

Hatimaye saa tisa ikawadia,nilichoka,na sasa ilikuwa ni safari ya kurudi,nikajizoa zoa na kushika njia kurudi nyumbani,bahati nzuri barabara hii ilikuwa na taa hivyo ikawa ahueni kwangu.

Baada ya mwendo wa dakika arobaini hivi nikahisi kama kwamba kulikuwa na mtu nyuma yangu,nikageuka kwa kasi, ebo! Nikaona nguo ya rangi ya khaki,aidha gauni au kanzu ikiishia na kufutika machoni kwangu....

Mshtuko uluonipata ukanifanya hata nguvu za miguu ziniishie nikajikuta nikiketi katika mfereji mfupi uliojengwa pembeni ya barabara.

"Ni nini hiki? Ni kweli au ni mawazo yangu tu?" Nikajiuliza,nukatazama huku na huko hali ni shwari,labda niliangalia vibaya bwana nikajizoazoa na kuendelea na safari..

Kiroja kingine tena! Ati nina vivuli viwili,kimoja ni changu na kimoja kimevaa kanzu kama si gauni!(mataa ya barabarani yanawaka hivyo mtu akipita kivuli chake kinaonekana kwa ufasaha kabisa) nikatetemeka kwa woga,nikageuka nyuma ati nacho kikageuka! Nikawa natembea kwa kurudi kinyume nyume,ati nacho kinarudi kinyume nyume!.



Lakini mbona kivuli changu kupo mbele yangu hiki cha nyuma ni cha nani? Na tumeachana umbali wa hatua kama tatu hivi toka kilipo hadi nilipo,nikaona huu sasa utani,nikifa si nife tu ebo! Nikakata shauri kukifuata he! Ati nacho kinageuza kila nikikifuata nacho kinaenda nyuma zaidi,ikabidi nikikimbize sasa..kikapotea.

Nikageuka na kuanza kukimbia kwa taratibu mithiri ya mbio za riadha,nikachoka nikaanza kutembea baada ya mwemdo mrefu kivuli kile kikarudi! Sikusimama nikaendelea kutembea tu.

Hata hivyo nikaanza kuhisi mwili kuchoka sana,miguu inauma na usingizi ni mwingi sana,nikajikalisha juu ya ukingo wa karavati kutafuta pumzi maana ilikuwa ni safari ya masaa mawili zaidi hadi nifike nyumbani...nikaanza kusinzia na hatinaye fahamu zikakomea hapo.

Kelele za watoto wakicheza ndizo zilizonigutusha,nikafumbua macho..afanalek! Nilikuwa nimelala chumbani kwangu..miguu ilikuwa imevimba kiasi na mwili mzima ulikuwa unaniuma...



"Lakini mimi mbona nilikuwa kule barabarani?" Nikajiuliza nisijue kilichotokea,nikaamka na kulibinua bati ninalotumia kama mlango,nikapenyeza kiubavuubavu hadi nje.

Nikawatazama nyusoni niliowakuta nje,wapo kawaida,hawana hata habari,pengine niliokotwa na wasamaria wema! Lakini mbona watu wapo kawaida kama hakuna kitu?...nikashindwa kuvumilia nikaamua kumuuliza mama ni muda gani niliingia kulala!

Akanijibu "we si uliingia kulala saa nne weww? Maswali gani hayo usinisumbue" ni nani aloyenirudisha nyumbani,na kile kivuli ni kiumbe gani? Je ndicho kilichonirudisha nyumbani? Lakini hakijanidhuru, hili ni fumbo niishilo nalo hata sasa kuna wakati natamani kukiona tena kivuli kile kilichovalia kanzu au gauni lililopauka lakini hakitokei tena.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 91

   




 Binafsi sijawahi kutana na hayo mauzauza, na ninaomba MUNGU nisikutane nayo maana nitakufa hapo hapo. Ila kuna visa viwili nilihadithiwa na wazee wangu.

Cha kwanza ni baba yangu mzazi, wakati akiwa kijana barobaro alikuwa anapenda sana kutembea usiku. Alikuwa anaishi maeneo ya Tegeta. Siku moja wakati anarudi usiku akiwa anatembea akawa anasikia kama kuna mtu nyuma yake anamfuata ila akigeuka hamuoni, akakaza mpaka akafika magetoni. Akajiandaa kulala akafunga mlango na kuzima taa akapanda kitandani.

Wakati bado usingizi haujampitia vizuri akawa anahisi kama mtu anafungua mlango kwa nje anamchungulia, akapotezea akalala. Katikati ya usingizi akahisi kukabwa na mtu akiwa amelala, akajitahidi kujitetea lakini bado, akajaribu kupapasa akahisi ameshika jitu lenye manyoya mengi sana mikononi kama manyani yale. Hapo ndo akajua shit just got real. Akaamka akawasha taa hakulala mpaka asubuhi. Alikuja kusaidiwa na mzee mmoja hv alikuwa anakaa mwenge almaarufu kama Babu wa Mwenge marehemu. Akamwambia lilikuwa jini alikumbana nalo njiani. Lakini bado since then hakukoma kutembea usiku.



Cha pili ni mama yangu. Ni mchaga wa rombo, anakwambia zamani walipokuwa mabinti wadogo kulikuwa na majitu yanaitwa "Mangauneri" wajuzi mtanisaidia. Walikuwa kama binadamu tu wanakuja hadi nyumbani mnakula nao chakula cha usiku ila wanakijiji walikuwa wanayajua kwa hiyo wanamkaribisha tu akimaliza chakula anaaga anaondoka. Sasa baada ya hapo ni kuwasha moto mkubwa maana akiondoka anasikilizia mkishalala anakuja anachukua vijinga anawachoma navyo especially matakoni. Waliokuwa wanapasua mbao porini walikuwa wanakutana nao sana.





Wednesday, November 2, 2022

USHUHUDA WA KWELI NAMBA 25.

   




ilikuwa 2002,tunatoka dar tunakwenda mkoa wa kigoma kwa wanojua bara bara enzi hizo wanajua ni jinsi gani kulikuwa na majambazi hasa ndani ya mapori ya Tabora,bahati haikuwa yetu mida ya saa 5 usiku wakati tupo road tukakuta bara bara imewekwa bonge la gogo mzee akataka kujitahid aligeuze ghafla walitokea watu wamebeba bunduki ndo kwa mara yangu ya kwanza kuone mtu kashka bunduki huku kajizungushia mkanda wa risasi mwilini bro wangu ile kuwaona tu akakata moto tuliokuwa hatujazmia tulikuwa watatu 3 mimi mzee na bimkubwa.



Tulichezea sana vitasa mzee alidhalilika mno mwisho wa siku walichukua mpka viatu nakumbuka viatu vyangu vya kitoto vya kuwaka taa,then wakaondoka mpka na gari tulikaa pale mpka saa 11 ndo tukapata msaada tukaenda polisi but hawakuwa na msaada mzee akapiga simu kigoma ikatumwa nauli tukaenda moja kwa moja mpka kwa baba yake(means babu),sasa babu yeye kila alivyokuwa anahadithiwa alikuwa anacheka mno hasa akimuangalia bro na ujanja wake ote et kazimia,upande wa baba yeye alikuwa na hasira mno alichokuwa anataka yeye ni wale watu awashikishe adabu hata kufa wafe basi ilivyofika usiku tukaelekea sehemu fulani inaitwa ujiji kwa mzee fulani alikuwa anaitwa juma njemba.



Nadhani kwa watu wa kigoma wanaweza kuwa wanamjua,akaelezewa kila kitu akasema hicho ni kitu kidogo sana,huku na yeye anacheka kisha akasema kuwa pale kwake kuna mbuzi alimchinja sababu ya sherwhe ya mwanae hvyo itatubidi tumtafutie mbuzi mwengne amreplace ili iwe kama malipo yake baba akakubali,kilichofata akawaita wajukuu zake walete (ubumba) ni udongo fulani hivi wa mfinyanzi kisha akawa anatengeneza kimdoli kidogo cha udongo kama vile vya kitoto toto,baada ya kukitengeneza akaanza kukiandika maneno yake kisha akakisimamisha chini,then akaanza kuongea maneno yake aliongea sana baada kama ya saa 1 akasema mtu yoyote ndani ya hichi chumba haruhusiwi kukimbia wala kupiga kelele kwani kwa kufanya hivyo ndo itakuwa kifo chake.



Basi aliendele kusema maneno yake ghafla yule mdoli pole pole alianza kukua na kuwa mkubwa pole pole,baada kama ya dakika arobaini alikuwa ni mkubwa kama binadamu mwenye mwili mkubwa alikuwa anamkono na kifua kikubwa na mrefu,kwa mara ya pili bro tena akazimia kwa mara ya pili mim mkojo ulishantoka natetemeka kama nmepatwa na dege dege,mwisho yule mdoli akaambiwa shtaka letu kisha akaambiwa nenda hivi vitu vinatakiwa leo leo,theb yule mtu akafungua mlango akatoka mbio alikuwa ni mwanaume lakini yupo uchi na ni mweusi tii kama mkaa mpka macho hakuwa na ichi kiini cheupe ye alikuwa na kiini cha moja kwa moja cha weusi,alivyoondoka tukaanza kumpepea na kumwagia maji bro alivyoshtuka yule mzee akatuambia kazi imeshakwisha kesho mtayapata majibu yenu.



Ilivyofika asubuhi tukapigiwa simu nakumbuka enzi hizo kulikuwa kuna buzz siyo hii tigo na hata simu zilikuwa za mezani,tukaambiwa kuwa kuna gari imepatikana Tabora yenye namba kama tuliyoripoti pamoja na vitu vingine,tukaanza safari na treni mpka tabora kufika kule tukakuta vitu vyetu na vingne vingi tu ila mzee alisema vyote vilikuwa vyetu hela zilikuwa kama 1m lakini zilipatikana 7m polisi hawakuchukua hata cent na hata walivyopewa walikataa kata kata hakikupotea hata kifungo kisha baada ya kuchukua tukaambiwa kuwa hao majambazi waliotuibia walikutwa msituni wakiwa wameuwawa wakasema wanahisi ni wanyama wakali ndo waliwauwa maana walikuwa wanaalama za meno makali milini mwao na kucha.



lakini wakashndwa kuelewa kama ni wanyama ndo waliwashambulia ni wanyama aina gani na kwanini hawakuwapiga hata risasi moja hao wanyama na wakati walikuwa na silaha nzito?Baada ya maelezo mengi mzee akawasha gari mpka kigoma stend ya kwanza mpka kwa yule mganga tulinunua mbuzi na zawadi nyingne nying lakini mzee aligoma hakutaka chochote zaidi ya mbuzi tu,basi tukampka mbuzi wake, akasema imebaki kazi moja tu na kazi yenyewe ni kumrudisha yule kiumbe(mdoli mtu)ili asitudhuru na sisi maana ni wetu hapo mdipo ilipokuwa mtihani maana kuna msharti mengi tulikosea plus kujisahau sasa akawa anatuandama sisi atuue dah kila mmoja nyumbani anaalama ya yule kiumbe yangu ni kungatwa skio na kula kipande nikipata mda ntawamalizia kisa changu but mpka leo mimi kwenda kwa waganga ni big no,but thanks god tulitoka salama



BLOG