Search This Blog

Thursday, November 3, 2022

USHUHUDA WA KWELI NAMBA 120

    




Mwaka 2002 nikiwa bado yanki wa chekechea tu nina miaka yangu saba nilikuwa na katabia kamoja matata sana. Wazee wangu wanapotoka then wananiambia nibaki nilikuwa nakubali then nawafuatilia nyuma wakifika mbali sana najitokeza kwa vile ni mbali wanakosa jinsi inabidi twende wote tu. Tulikuwa tunaishi ubungo msewe kwa chini kidogo,kwenye lile ghorofa la Tanesco lililovunjwa,ukivuka barabara na kuteremkia bondeni,unavuka mto kisha ukupandisha unakutana na uwanja wa mpira,kushoto mwa uwanja kuna makaburi na katikati ya makaburi kuna njia ndogo ya mkato.



Mandhari ya eneo la makabuli,kulia kuna nyumba mbili ama tatu hivi zimejengwa kuzunguka makaburi,kuna vichaka vya maua na miti ya vivuli,kushoto kuna nyumba moja kubwa ya kifahari,miti ya maua na vivuli inakutana katikati ya njia,njia hii ina ukubwa wa hatua mbili hivi za mtu mzima,kingo zake zimepandwa maua,njia inayagawa makaburi katika sehemu mbili zilizo sawia.





Miti hii kwa juu imeshonana kiasi na kufanya njia iwe mfano wa barabara zinazotobolewa katikati ya mwamba au mlima(Tunel)sehemu ya kuingilia imepambwa kwa maua na kuwa kama mlango wa pango hivi sawia na upande wa pili wa kutokea eneo hili(ilichagizwa na maua yanayotambaa kama mapesheni siyajua jina lake maua yametambaa juu ya miti) Basi hiyo siku nimeona wazazi wangu wanajiandaa kutoka kwenda kwenye harusi ,Mikocheni na sijataarifiwa na mimi nijiandae,nikaelewa! Nikachukua nguo nzuri(mayanki wa kipindi hiko wanaelewa maana ya nguo nzuri) nikazificha nje pamoja na viatu,nikawangojea watoke na mimi nikatoka,nikavaa chap na kuamza kuwafuata nyuma,huo muda ilikuwa saa mbili usiku kuelekea saa tatu. Nikiwa nimewaacha umbali wa kama hatua kumi hivi,mwendo wa dakika tano tu ulitosha kutufikisha eneo la makaburi,nikasimama na kuwaacha waingie kuvuka nikawahesabia timing kuwa washavuka na mimi ndio nikaanza kuvuka.



Kwa vile nyumba zile tatu hazikuwa mbali sana mwanga wa taa uliangazia kidogo sana eneo hili,nikaanza kupiga hatua,harufu kali ya marashi ambayo hadi leo sijawahi kuyasikia niliyasikia vizuri sana,ile kutupa macho mbele namuona msichana mburushi,sijui mwarabu kasimama tuli pembeni ya njia ananiangalia ninavyozidi kumkaribia. Nywele zake zilikuwa ni nyeusi na ndefu karibia kugusa kiuno,gauni jeusi lenye mng'ao hafifu,midomo ilikuwa na lipstick nyekundu,macho makubwa meupe na alikuwa amefumbata mikono yake kwa kuipishanisha kifuani kama wafanyavyo mabosi wengi wa mjini. Kiroja kikaanzia hapa,kadiri navyomkaribia naye alikuwa anaongezeka urefu,wakati alikuwa mfupi kiasi lakini hadi namfikia ili nimpite tayari asingeweza hata kupita mlangoni labda kwa kuinama kidogo.



Nikamfikia na kumsalimia shikamoo,akaitikia mar habaaaa,wakati huo nimegeuza shingo juu kumtazama naye alinitazama,baada ya kumpita na na kumwacha hatua kama tano hivi,hizo mbio nilizotoka nazo kwakweli sikumbuki kuwahi kuzikimbia mbio kama zile. Nikaliacha eneo la makaburi na kuteremka bondeni,nikavuka kidaraja na kupandisha barabarani,nikawasili kituoni(hiki kituo kwa mbele ndio unatazamana na jengo la Tanesco lililovunjwa,ile kutazama huku na huko wazee siwaoni na watu ni wengi,kiasi kwamba watu wakaamza kuhisi nimepotea wakataka wanishike wanihoji vizuri,nikawaponyoka nikashusha bondeni ili nirudi nyumbani. Hatimaye nikafika eneo la makaburi,nikasimama nikijishauri kupita,moyo wangu uligoma,ulikataa katakata na hapo inaelekea saa nne na nusu usiku,nilichokifanya ni kuzunguka njia ndefu kwelikweli,nilitumia lisaa na nusu kuzunguka wakati kama ningekatiza makaburini ingekuwa safari ya dakika kumi tu!





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 119

    




Haahah,kuna kisa cha mpemba Mafia, alikua ameanika samaki wake baada ya kuwavua, ikafika mda akatoa mkeka akawa anapiga rakaa(Anaswali).Amemaliza kuswali kugeuka hamadi samaki wake wawili hawapo, akauliza kuna ntuu kachukua samaki zangu arudishee kila mtu akakakana akasema mi natoa dakika kumi tuu msiporudisha Walah! atakufa mtuu hapa na si masiharaa... Ebanaeee baaada ya dakika 10 zikaanguka kunguru mbili(hawa ndege Weusi) zimeshakaukaa zamani mdomoni wanamabaki ya samaki....





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 118

    



Na huko kuelekea Lukozi ndio kuna msitu unaitwa 'kandele ka paa' huko ndio kuna mapicha sio ya nchi hii, waulize waendesha magarii...



Na ukitokea huko mkuzi...

kimbembe kipo pale kati ya msitu kwenye daraja flan kubwa, maji yanayopita ni mengi ila yanashuka taratbu, kila upande ni giza kubwa si barabarani sio msituni maana maeneo hayo ndio msitu umefura kisawa sawa na miti ni mikubwa mirefuuu kwaio hata mwanga wa jua haupenyi...



Kwaio pana sifa ya Ukimya, giza kubwa, msitu mnene, Daraja kubwa lenye maji mengi,

You can imagine....



pale Hata walevi wakipita wanaacha kelele kwanza.. ndio utajua Pombe inaogopa nayo..

Maji yenyewe hayapigi kelele wala ndege wa polini wewe upge kelele ni nani?....

Pametokea matukio mengi sanaaa.....



Yote kwa yotee yale maeneo yana mapicha picha sanaaaa...

Huko huko mkuzi kuna mzungu mmoja maarufu sana naamini hata wewe unamfahamu, alikua anaitwa mzuka,



Kisa cha kupewa hili jina ni kwamba alikua na shamba akaambiwa popote utakapoona huu mti usiukate ni makazi ya majini/shetani..

Akapuuza siku akaukata...

Alikula bonge ya banzi, kuanzia pale akawa amepinda shingo, kichwa kimelalia upande mmoja...



Maisha yake yote yaliobaki alikua akitembea na kikapu kilichojaa mawe upande mmoja ili ku balance mwili maana ulikua umelala upande mmoja...



Pia tushawahi pita sehemu usiku miti ikalala yoteee.....

Pia mzee alishawahi salimiwa na vibwengo usiku akitoka magamba coast akipita ule uchocholo wa magamba sec...

Akavitukana sana huku anachomoka kasi ya ajabuu..

alifika nyumbn hana kiatu kimoja.....



Kuna mapicha mengi sanaa kulee....

Yale maeneo yote yalikua makazi ya wajerumanii,

nyumba nyingi km ya mkapa, ngwirizi na majumba mengi sana yamejaa...



Hata sisi kambi yetu ilijengwa na mjerumanii,

Majumba yao yamedizainiwa kiajabu sanaa....

Tumeish kwenye nyumba miaka na miakaaa,

eti tunakaribia kuhama ndio tunajua tunaishi juu..

kumbe chini kuna nyumb nyingne yenye mavyumba na hapo barazani chini kumbe ni bonge ya kisima..



Ilikua ukizunguka msituni kukuta sehemu imesakafiwa au makorokocho korokocho mengi ni kitu cha kawaidaaa..



Nimepamisss long time sanaaaa..





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 117

    




Alikuwepo mfanya biashara mmoja huko(alikuwa anafanya biashara za magendo) basi kila alipokuwa anapita na pikipiki yake akawa anasumbuliwa na askari mmoja wa barabarani ikabidi awe anatoa hongo ili asikamatwe ilifika time akachoka kutoa hongo.



Siku mmoja akapita kama kawa akasimamishwa na yuleyule askari. Alikuwa na ndoo amefunga kwenye pikipiki yule askari akaenda kukagua haaa akakutana na kichwa cha mtu kinatoa damu mbichi kana kwamba kimekatwa muda huohuo.



Askari aliruka kwa mshtuko maana hakutarajia kuona kitu kama hicho wenzake kufika pale kwenye ndoo hawaoni kitu.



Unaambiwa alitoka pale moja kwa moja kuomba uhamisho kurudi kwao.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 116

    




Mwaka fulani nikiwa katika mafunzo ya JKT katika kambi moja wapo hapo Kigoma,

Kuna ServiceMan mwenzetu alimua kapangiwa lindo huko ndichi mashamani, mchana akiwa lindoni akakutana na bibi kabeba mkungu wa ndizi za jeshi, Basi Service akachukua ndizi na bibi akarushwa sana kichura, mwendo wa bata na kupiga push za kutosha kisha akaachiwa andoke zake.



Jioni jamaa anarudi Hangani(Dom) baada ya kukabidhi silaha akaanza kuumwa sana mpaka asubu ni mahututi, hospitali wanadai hawaoni ugonjwa basi Nyumbani kwao wakamuomba akaenda kutibiwa na akapona, Siku anarudi kambini ile hali inaanza upya, akitoka nje ya kambi mzima ila akiingia kambini hoi. Mpaka Utawala wakamumisha Kambi.



Shkmaooo Kigoma.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 115

    





Kama mtaikumbuka ile mvua ya mawe kahama march 2015 ngoja niwape kisa chake.



Mvua zilikuwa adimu sana basi wananzengo wakamfuata mganga mmoja alokuwa ana tuhma za kuzuia mvua

Basi watu wakamuhoji akakataa tuhuma hizo. Jamaa hawajaelewa wakampiga hadi kumuua.

Wakati anakufa alisema nakuta lkn mtaona.

Waloelewa walianza kuhama walokaza shingo wakakomaa .....

Mvua ilipoanza wakasema tumemuua yule alikuwa anazuia mvua....lkn ikaja kuzidi....na mawe juu. Iliua watu na mifugo na uharibifu mkubwa ulotokea.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 114

    





Wale waliosoma boarding mnamkumbuka miss corridor sjui nyie mlimwiitaje in short huyu ni jini huwa anatembea ukumbuni kwenye mabweni mashuleni au makambini au maholi tulitunga hilo jina sababu akitembea unaskia "ko, ko, ko " ile sauti kama ya viatu vya kike vyenye visigini virefu ukienda angalia huoni mtu ukibahatika unamuona mwanamke ana nywele ndefu kakupa mgongo anamalizia kukata kona

 miss corridor,, umenikumbusha mbali sana.. vyooni kulikuwa hakuendeki usiku hata mbebane kumi mkisikia hiyo "ko" au mlango umejibamiza "pa" wote mnatoka nduki kila mtu na hamsini zake,, chumba kilicho karibu yako ndiyo unaingia unajibanza humo humo hamna kuulizana tutajuana asubuhi.. wallahi maisha ya boarding kuna muda yananifanya namiss sana skuli

 





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 113.

     






Kisa hiki kilitokea mbuga ya katavi ambayo sasa ni mkoa, kuna mzungu alinunua kitaru kwa ajiri ya kuwinda wanyama. sasa siku moja akaenda kuangalia kitaru chake akiongozana na askari pamoja na wazungu wenzie Ile kufika akamkuta Mzee mmoja anatoka kwenye kitaru chake huku kabeba mnyama begani. Mule kwenye gari walibaki baadhi ya askari, inabidi askari wamwamulu Mzee kunyosha mikono juu na kuelekea kwenye gari ile kugeuka tu gari haipo pamoja na watu waluomo Ndani ya gari. mzungu akuamini kilichotokea inabidi amruhusu Mzee aende na myama ile mzee anaondoka gari ikaonekana ipo pale pale.






USHUHUDA WA KWELI NAMBA 112

    




Kuna rafiki etu mmoja walikuwa na party koko beach,sasa yeye ni mnywaji wa pombe zote.sasa akiwa coco beach akaja muhudumu àkamletea soda,jamaa akamfokea wewe mimi nimeagiza kitu fulañi na sio soda.yule mwanamke ambaye ni muhudumu àkàmsogelea na kumfungulia huku akimwàmbia utàkunywa soda.

Muda huo ni yeye ndie anayemuona muhudumu wale wenĹşie hawamuoni.

Baada ya muda ndugu zake wanamuona kaka yao àkiogelea kweñda kati kati ya bahari,sasa wao wanamshangaa si ameagiza kinywàji na kuogelea hajui anaogeleaje kufika kule (maji mengi) .Wakainuka na kuañz kumkimbilia huku wakimwita jina lake jamaa hakugeuka wakamwita sana hakugeuka mara àka wapotea baharini.

POLISI na familia Ĺşikamtafuta kando wa mbambao siku tatu jĂ maaa hakuonekana hai wala mĂ iti.siku ya tatu usiku ndio jamaa kaja mwenyewe anajokokota hajiwezi na kufika nchi kavu akadondoka.wĂ tu kumuokota muhimbili.

Alipopona ndio akatusimulia kuwà baada ya kukataa soda yule mwanamke alikasirika sana na akamchukua na kwenda nae baharini çhini kabisa kuna mwamba ambao walikuwa wàkibishana muda wote .yule mwanamke alikuwa anamwambia kuwa anampenda na jamaa alikuwa na msimamo wa kumkataa na alivutwa kutaka kuelekea chini ya mwamba zaidi ndio jamaa alijizatiti ende zaidi na wamepambana muda wote mwishowe yule mwanamke àka mwambia una bahati mizimu ta kwenu ina nguvu na imekulinda.

akaçhwa ,jamàa akawa ana hangaika kupanda ule mwamba wa mawe maana alikuwa ànaona njia ya kutoka shida ni kupanda amehangaika kupanda juu wabmwamba wa jiwe mpaka akatoka.ndio kutoka amepoteza fahamu.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 111

    






I remember back in the days in the village when i used to trick boda guys..because our house was close to a cemetery.Once i climbed the bike i would stuff my nostrils with cottonwool without him knowing. Then when we got infront of the cemetery i would scare him and he would run for his life! On this fateful day, i boarded the bike as usual and stuffed my nostrils with cottonwool.when we got to the cemetry i scared him but this time he just stared at me.I danced all the ghost songs i know..but he didnt even move.I even spoke pidgin "oga..you no dey fear ghost!?" nothing happened.He got up and held my shirt "nipatie pesa zangu mjinga ii" I begged the guy to calm down and let me get it for him..i went into the cemetry as he held my shirt and followed me.As i was walking..i jokingly knelt down on a grave and knocked on it "Habari..nsaidie na 200 nipatie hii ghasia iniachilie" i thought this would scare the guy..but nothing! kidogo kidogo a hand stretched out from the grave holding 200/- note "chukua hii na unirudishie ukipata" My brothers and sisters..to date..i still dont know who carried who between me and the bikeman out of that cemetry.ile kitu nakumbuka tu ni nilijipata juu ya pikipiki at a neighbouring town.As for the bikeman sijui alienda wapi..i still have the bike parked at home .whenever i pass by that place,i always see my one pair of gucci shoe that fell off as i was running .It is not that i cannot go and get it oooo...just that i dont like gucci stuff anymore.Infact..i dont like shoes again!! 















USHUHUDA WA KWELI NAMBA 110

    






Nikiwa dodoma mtaa wa chang'ombe mwaka 2000 nilikua na rafiki mmoja ambae baba alikua mwanajesh(mzigua) na mama nesi ,wazazi wa huyo rafiki niliekua nae walitumia stuli kuhifadhia pesa,ilizibwa pande zote kwa vipande vya sealing board,

Wakati wa likizo moja ya mwezi wa sita ,huyo fafiki yangu alikua akija na pesa na tukatumia kwa mambo tuliojua wenyewe kwa wakati huo,

Alikua akiiba pesa kwa zaidi ya wiki tatu,jioni moja alipanga kuleta pesa ili twende club moja maarufu kama NK ,alikamatwa na bibi yake akitokea chumbani kwa wazazi wake na pesa,



Baada ya baba kurudi kazini ilikua ni kipigo cha mbwa mwizi,

Siku moja baada ya kipigo kwa huyo rafiki yangu nilifuatwa asubuhi na bibi yake akitaka nimpe kila alichoninunulia mjukuu wake,mimi nikatoa saa niliyokua nimevaa mkononi na kumkabidhi



Kilichofuata ni kuumwa magonjwa yasioeleweka,kila hospital walisema hawaoni kitu,ilikua navimba kiungo kimoja baada ya kimoja kwa kulala tu ,hata kama ni mara nne kwa siku bas nitavimba sehemu nne tofauti.

Niliish na mama wa kambo peke yake wakati huo huku mzazi wangu(baba) akiwa safarini kikazi,

Ilimbidi atafute njia mbadala (mtaalamu wa jadi) ili niweze kupona.




USHUHUDA WA KWELI NAMBA 109

    






Uchawi ni kweli Upo, Nikiwa Nimeenda Kurudia Shule Baada ya kukosa Nafasi ya kujiunga Form One 1994..Baba yangu Mkubwa..Tumbo moja na Baba Alikuwa anafundisha Shule ya Msingi Nyabhutanga Jimbo La Buchosa wilaya ya Sengerema 1990--1995.. Mzee wangu Alikuwa Anatembeza Bakora kama hana Akili nzuri siku moja Akachapa mwanafunzi wa Darasa la 6 na inasemekana Alikuwa hachapwi na walimu sababu ya Mama yake kuogopwa kwa Uchawi.. sasa baada ya Kwenda kushitaki kwa Mother yake, Saa 2 Usiku mother mtu Alikuja kumuonya Mzee wangu Home Asirudie tena kumchapa Binti yake.. Mzee Akamwambia Asimtishe na Asirudie tena kuja kumletea vitisho..



Siku nyingine tena Miezi kama 3 Baada ya Tukio la mwanzo.. Yule Binti sijui Alikosea nini bhana Mzee Akamcharaza tena Bakora za Kutosha, mother usiku saa 1 Akaibuka home Kwetu Akamfokea sana Mzee wangu na kumuonya tena, Sasa Ba mkubwa Alivyokuwa mbishi sijui nini kilimpa si Akamdaka yule mother Akaanza kumtembezea Bakora za kutosha hadi walimu Jirani wanakuja kuamua Alikuwa Amemvuruga sana.. Hakwenda Polisi wala Hospital Alijiuguza hadi Akapona.. mwisho kwa Ile Fedheha Akahama Kijiji. Lakini mwaka Mmoja Baadae Ba mkubwa Akiwa Anakunywa Pombe kijiji Jirani cha Bukokwa Alishangaa Kumuona Yule mother Akiwa miongoni mwa wahudumu, Akashangaa Sana Ile bado Akiwa hajui La kufanya Akamwambia Afanye Matengenezo ya maisha yake Kisha ghafla kama upepo Akapotea.. Ba mkubwa Akiwa na Pombe kidogo kichwani Alimpuuza Lakini Alikuja Kutusimulia Kesho yake..



Baada ya Mwezi mmoja Ba mkubwa Akiwa Anatoka Kijiji cha Sukuma Akija Nyabhutanga Usiku Kama Saa 6 hivi Akiwa Anaendesha Baiskeli Ghafla Aliona Fuso Linakuja kwa kasi(Na kwa siku hiyo huo muda Hakuna Gari lilikokuja hapo kijijini kwa muda huo) Alijaribu kulikwepa na Kuishia kuanguka na kupoteza Faham. Alikaa Sengerema Hosptl miezi 3 baadae Tukamhamishia Bugando..Baada ya miezi 3 Akiwa Bugando Hospital Alifariki.. Huwa Naumia sana Kila nikitafakari tukio Hilo Maana Nilikuwa Nasomea Hapo kwake na Ndo Alikuwa kila kitu kwangu kwa wakati huo..





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 108

    





Kisa changu mimi, nakumbuka mwaka 2011 nilipata kazi, ikanibidi nihame home nitafute getho. Nikapata ghetto la bei rahisi chumba sebule sehemu moja inaitwa "Kwa Ali Mboa". Huko Jeti lumo kama unaelekea airport hapa mjini daslama.



Kuna siku nimetulia sebleni usiku nacheki movie, mara nikapitiwa na usingizi makali ghafla. Nikiwa usingizini nikamuona mke wa jirani yangu anaingia ndani kwangu kajifunga kitambaa cheusi kifupi, akanifata kwenye kochi nilipokuwa nimejilaza, akanikanyaga kifuani, akageuka tena akataka kunikalia usoni. Wakati anataka nikalia nilisikia harufu mbaya sana inatokea kwenye private parts zake(sijui ni anus ama vagina). Nilihangaika hadi nikashtuka usingizini...nikajisemea, itakuwa ni ndoto tu hiyo. Mara nikapitiwa tena na usngizi mkali. Mara hii nilikaona katoto ka jirani yangu kanaingia ndani kwangu kakiwa kamejifunika kitu cheusi kama shuka jepesi kuanzia kifuani.



Hizi ndoto zikikuwa zinajirudia karibu kila nikilala lakini naona watu tofauti tofauti ninaowafahamu. Wengi wao wakiwa majirani zangu.



Nilipohama hiyo sehemu, sikuwahi kuota hizo ndoto tena. najiulizaga bila majibu kama zile zilikuwaga ni ndoto ama ni wachawi waliokuwa akinijaribu!!



Majirani zangu wote walikuwa wamakonde.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 107

    




Mimi na mshkj wng niliwahi kuenda kwa mtaalam mmoja nilimsindikiza uyo mshkj wng mimi nilikuwa sina imani na nguvu za giza insuch kipindi iko afu nilikuwa mbishi, sas bana yule mzee alisema kimasihara kuwa kuna dawa nikiwapa unaona wachaw na majin usiku, mshkj wng aliogopa akaikataa mm kwa kiherehere changu niliiomba uku nikijichekesha nakudhan ni mchezo wa kuigiza. Alinipa akaniambia hii utaoga usiku alafu na hii utaipaka kabla ya kulala afu hii kesho asubuhi utaogea na kupaka ili kuiondoa iyo hali ya kuendelea kuona ila sharti ni moyo usizungumze chochote pindi utakapokuwa uona ukizungumza utajijengea mazingira ya uadui..nikakubali, Haha ayse yanii ule usiku siusahau kwa vituko nilivyokuwa naviona dunia ina mambo mengi nyiny zaidi ya unavyoiona..



Nilikuwa naskia kwenye kordo mtu anatembea kuja usawa wa chumba tulicholala akivalia viatu vya mchechemea mara mlango unafunguliwa haingii mtu unaingia upepo tuu. Nikimuuliza mwenzangu anasema hajaskia mlango ukifunguliwa ninamawange amna kitu. Nilianza kupata kausingiz baada ya muda niliskia kishindo kwenye bati yan kwa kile kishindo ni kama uzito wa gari umeshuka juu ya bati mpaka nikawa nachungulia nakujiuliza iki kitu kwa kishindo iki hakijaingia ndan kwel nikimchek mwenzangu hata hajashtuka chochote kwa kile kishindo ndo kwanz anauchapa usingz na kukoroma, yalitokea matukio kadhaa kadhaa ila kubwa zaidi ilifika mda nkapitiwa tn na usingiz nkawa naota km kitanda iv kimeinuliwa juu nikashtuka kiaina ile nimefungu macho naona cyling body hii apa karb ni kitendo cha kunyanyua mkono na kuishika tuu nimepigwa na bumbuaz flan sekunde kadhaa nachek tn naona kitanda kipo fresh chini. Yan we acha tuu nilikoma usiskia mtu anasumbuliwa na mauza uza iv vitu ni hatar mnoo. Mara uskie ngoma nje zinapigwa mapaka yanalia kupitiliza yan af asbh nikiuliza wanasema hakukuna na milio ya paka jana





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 106

    




Tukio LA kweli

Kisiwani kome ziwa Victoria mkoani Mwanza.

Baba yangu mzazi alitoka Mwanza na mkewe mama yetu mdogo wakaelekea kisiwani kome kutafuta mahali pazuri pa kufanya biashara na shughuli za uvuvi,walikuwa wanamiliki boti na wanafanya kazi wakiume kwa ajili ya kazi za boti,na alikuwepo mama mmoja aliyekuwa mpishi katika hiyo kambi ya faza...sasa Mimi na Dada yangu tukapelekwa kuishi na faza huko kisiwani sasa mambo yakaanza...

Jirani ya kambi alikuwepo Mzee mmoja anaishi umbali kidogo na kambi yetu,nyumba Yake ilikuwa katikati ya migomba palikuwa panatisha balaa mchana lakini kulikuwa na giza kama usiku,kumbe yule Mzee ni mchawi Wa kutupa,akajifanya rafiki mkarimu na kina faza...hadi sisi tukawa tunapenda kwenda kwake kuchukua pilipili,ndizi na viazi...akiondoka anaacha ujumbe pale kambini watoto waje kuchukua viazi tunaenda.

Huyu Mzee alikuwa muumini nzuri Wa kikristo akawa anaenda kanisani kila jumapili hakosi.

Sasa kumbe yule Mzee alikuwa anampenda yule mama mpishi,kila akimwambia yule mama akawa anamkataa hamtaki kwa kuwa ni Mzee..sasa alichokifanya akatumia uchawi wake kumpata yule mama mpishi wetu kambini.



Siku moja jumapili Mzee akapita pale kambini akasalimia huku akiwa kwenye furaha kubwa sana ikionekana dhahiri usoni,akamwambia yule mpishi nenda nyumbani ukachimbe viazi mimi naenda kanisani..akamuelekeza na matuta kabisa..kumbe alikuwa ameshatega mitambo Yake...yule mama kufika bahati nzuri au mbaya alikwenda peke yake hakuenda na sisi maana tulikuwa tunatembea nae kama mkoba.

Sasa alipofika akaanza kuchimba viazi kupiga jembe LA kwanza nyoka akamgonga mguuni..ile anajaribu kukimbia akamgonga tena kisha akapotea..mpaka Mara tatu akawa anapiga kelele kuomba msaada lakini wapi hakukuwa na MTU eneo lile au watu kusikia na kwenda kumsaidi mpaka akaamua kurudi kambini wakamfunga kitambaa ili sumu isipande mwilini na kusambaa...wakaja waganga wakienyeji kama watano kila mmoja anafanya utaalamu wake anashindwa mpaka akaja mganga Wa mwisho akampima kwa kutumia SAA ndogo..akasema mgonjwa ameshafariki kitambo sana,watu walilia sana,na yule Mzee alikuwepo anajifanya anatoa msaada kama msamari mwema.

Ikabidi maiti isafirishwe kwenda kuzikwa Mwanza mjini ,tulipanda boti na maiti kuelekea mwanza....kufika katikati ya ziwa mafuta yakaisha boti likaanza kupelekwa na upepo hovyo hovyo watu wakaanza kuomba dua zote mungu atuokoe maiti ifike salama na roho hai ziokoke!!!,Mungu saidia ikapita boti ya kishimba,wakaipungia mkono kwa mbali ikaja karibu na boti yetu..bahati nzuri faza aliwahi Fanya kazi na maboti hayo wakatusaidia mafuta ..tukafika salama mjini,maiti akazikwa salama msiba ukaisha.



Sasa baada ya siku kupita yule mama akawa anaonekana kwa yule babu mchawi wanaishi pamoja kama Mke na mume,ukimshitukia ukamuona yule mama anapotea...mpaka Leo sijui maisha yao yaliendelea vipi kichawichawi,kama walisha kufa au wapo hai Mungu ndiye mjuzi.

N.B

Ila Mzee alijipatia Mke kwa njia za kishirikina au giza!!!





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 105

    




Nimekumbuka hiki kisa,



Mbeya mjini nilikutana na kisanga cha kubebeshwa mkojo na wazee wanacheza drafti, bao na kunywa kahawa,

Unakuta wanacheza wewe unaenda shangaa pale (mimi nilikua nasubiri coaster za usiku za dar) nimeshangaa wee baada ya dk 20 hivi nkabanwa mkojo nkarudi kwa mwenyeji nkamuomba anielekeze pa kujisaidia, nimerudi kujisaidia naenda kushangaa na kuskiliza stori zao, yaani ndani ya lisaa nilienda chooni mara 3, nkawa najisemea mapema yote hii hata maji sijanywa mkojo mwingi hivi?

Kwa sababu nilikua na safari niliogopa kunywa maji japo nilikua na kiu sana kwa hofu ya kusumbua gari njiani kuchimba dawa,



Gari ilivyokuja nkaanza pakia carolight zangu nkamaliza nilipotaka kurudi pale kuendelea kushangaa mwenyeji wangu akaniambia twende huku (hapo tunasubiri gari ijae abiria) tukakaa mahali tunapiga stori za hapa na pale ndio akaniambia nimekuona unabebeshwa mikojo tu hata huelewi, nkabaki namshangaa...

Ndio akaniambia ukienda shangaa pale kama hauko vizuri wale wazee wakiskia mkojo wanakubebesha wewe unaenda kuukojoa badala yao, yaani wanaweza kukaa asubuhi hadi jioni hata chooni wasiende ila wee kila mda unapiga ruti tu..

Hiyo ilikua mwaka 2010 pale uyole.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 104

    



HII IMETOKEA JANA USIKU



Nipo kwenye kijiji kimoja kipo katika wilaya ya NKASI huku mkoa wa RUKWA



Mishale kama ya saa 12 hivi jioni(jana) alipita mzee mmoja anatafuta mbuzi wake ambae kwa maelezo yake ni kuwa ameibiwa...amepita sehemu nyingi tu hapa kijijini ikiwemo na sehemu ambayo mimi ninaishi "kuomba arudishiwe mbuzi wake"



Mishale kama ya saa 3 sasa,nimekaa zangu naangalia TV Zilipiga radi 2 za ghafla tu(hakuna wingu wala mvua ilionyesha baada ya hizo radi)



Asubuhi hii naenda sehemu yangu ya kazi,mfanyakazi mwenzangu ndo ananiambia zile radi za jana ZIMEPITA NA WATU WAWILI(kuua)





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 103

    



One day nikiwa darasa la nne hiv tulichezea stick kama zote sababu ya kuchelewa namba, usiku wa siku hiyo nikaongea na dogo langu yy alikuwa darasa la tatu kuwa siku inayofuata tuamke mapema,



Bhana weee majira kama ya saa nane/tisa mzee tuko hewan, tukajaza zetu maji kwenye galon (5lt) kila mmoja la kwake, ile tunatoka mzee akatuzingua kuwa ni mapema mno, so turud ndan,



Aaaaweee 2kamkubalia kwa kwenda ndan, then alipoingia kulala tuuu, tuakamsomea timing tukapita na mlango wa nyuma, then tukaelekea kiskul.



Bhana weee, njan tulikuwa pekee eeetu, njan tuliyopitia kwa asilimia kubwa imefunikwa na miti miref aina ya mikaratus, ucku ulikuwa ubatisha balaa,



Cha ajabu tupofika skul, hata mlinz hakuepo, coz tulimsaka kila anga, hakukuwa na mtu, tulikuwa tunasikia kama mtu anatwanga kitu kweny kinu, then mwingine kama ana nyanyua ndoo ya plastic then anaiachia inajipigiza, hatar sana.



Dogo alinambia niangalie sehem flan hiv kweny mti yy anadai anaona mtu amevaa nguo nyeup anapanda na kushuka, me macho yangu yaling'ang'ana na mwanga wa taa tuu, huku nimeshikilia dirisha.



Tuliposikia Swalaaaa, ikabidi tutafute darasa tukapiga mbonji then saa kumi na mbili unusu tukapata namba zetu, lkn cha ajabu siku hiyo ticha hakupiga wala nn.

Aaaaacha kabisa sintokuja sahau hii nshu.






USHUHUDA WA KWELI NAMBA 102

    




Anasimulia dereva wa Fuso Jangwani.



Hiyo siku wamekaa maskani kama kawaida wakisubiri wateja, haukupita muda akaja mzee wa kiarabu hivi(mburushi).



Mzee akaulizia huduma ya kupelekewa mizigo yake wanapopandia boti za kwenda Mafia, wapo waliomkatalia, akajitokeza kidume, akamwambia mzee twende. Akamwambia kuna vity vyangu nimenunua vingi viko Kariakoo, twende tuvipitie, swala la muda lisikupe tabu, nitakulipa kijana.



Huyu alikuwa ni mzee wa makamo kidogo, basi jamaa mpaka Kkoo, wakapakia safari ikaanza. Kufika pa kupandia boti, mzee akamwambia dereva sasa kijana wangu naomba unielewe hili, naomba twende nyumbani tuvuke pamoja nikakupe pesa yako, swala la muda wa kukuweka huku isikupe tabu. Dereva keshayavulia tena ikabidi akubali tu, safari ikaanza. Wamekwenda, boti ikafika pahala ni kwenye maji bado, yule mzee akamwambia muendeshaji kuwa simamisha hapo mi nimefika.



Kila mtu mle ndani haamin mzee anachokisema, mzee akawaambia simamisha, kweli nahodha wa chombo akatii, mzee akakuta wameshamsubiri tayari vijana wake, wakaanza kupakua mzigo ukaisha boti ikaendelea na safari. Sasa yule dereva akaamua kuwa mpole tu, akaambiwa na yule mzee kwa ukarimu kabisa, usiogope kijana karibu nyumbani, yule jomba akashukuru, wakaingia ndani, kwanza aliposhuka toka chomboni akaona bonge moja la mji, hajawahi fikiria kuliona. Kakirimiwa vizuri, akaambiwa ukitaka kuoa, njoo tu huku nina mabinti zangu hawajaolewa usiogope. Jamaa akapewa pesa yake akapelekwa pale pale aliposhukia akapandishwa chomboni mpaka ng'ambo. Baada ya tukio lile yule jomba hata umwambie nina mzigo nipelekee Temeke, humpeleki.






USHUHUDA WA KWELI NAMBA 101

    




Nimemkumbuka mwanangu pengo o level mkoa flan aliwahi kumuibia mzee mmoja iv km ustadh mwanangu pengo alikuwa kipofu yan haoni ndan ya week nzima huezi amini hospital walishindwa kujua tatizo, pongezi ticha mitomingi aka alijiongeza tukampeleka mwanetu kwa mtaalamu yai, nazi, sindano ndio vitu vilivyomfanya mwanangu aone tena ndan ya dk40. Tokea siku iyo nikiskia mtu ananiambia ntakuonyesha wew huwa nakuwa km piriton.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 100

    




Hiki kisa kilinitokea mimi mwenyewe miaka ya 80, kati ya 86/87. Sikumbuki mwaka sahihi sababu ya umri mdogo niliokuwa nao, ila nilikua najitambua. Tukio hilo lilitokea sehemu ambayo baadaye nilikuja kujua kuwa inaitwa makuburi jijini Dar, baada ya kuwauliza wazee nikiwa na umri wa kutosha kwenye miaka ya 90. Maana ni tukio ambalo hadi leo huwa tunataniana sana tukikutana familia nzima. Nakumbuka ilikuwa kipindi hicho Mzee alikuja Dar kwa ajili ya kusoma UDSM baada ya kuamua kujiendeleza. Sasa akaona ili asome vizuri, ni vema awe pamoja na familia yake. Kwahiyo baada ya kumaliza taratibu za kujisajili chuoni, akaamua kutafuta nyumba. Ndio akapata nyumba nzima huko makuburi. Basi akafuata familia yake, mama, mimi na dada yangu. Basi tukafika jijini Dar, na kuanza maisha mapya. Lakini hatukuchukua raundi, ndani ya mwezi mmoja tu. Ndio likatokea tukio hilo. Siku hiyo ilikuwa ni usiku mnene, sikumbuki ilikuwa ni wa saa ngapi. Ila nilikuwa sijapata usingizi bado. Hata dada angu alikuwa hajalala. Maana tulikuwa tunalala kitanda kimoja(mzungu wa nne). Pia tulikuwa tunalala na binti wa nyumba ya jirani, alimuomba bimkubwa ili atupe kampani maana tulikiwa wadogo kuliko yeye. Pia ni mwenyeji. Mimi kidume niko upande wangu kimya, nasubiria usingizi wakati wao wanapiga tu stori. Hapo tumeshazima taa yetu ya chemli. Nimekaaaa....mara ghafla nikashtuka naona mtu mweupe amesimama pembeni ya kitanda tena usawa wangu!! Nikashtuka, ila sikufanya chochote. Nikawa namtazama tu. Baadae nikamuona anaanza kutembea kukizunguka kitanda. Kapiga raundi moja kisha akakaa juu ya kingo za kitanda upande walikoweka vichwa dada na mwenzie. Mi namuangalia tu! Akapiga raundi ya pili, akakaa tena palepale! Ikabidi nimshtue sista,(nikamwita jina lake) mtu huyo!! Wakashtuka...wakaangaliaa...hawajaona kitu. Akanimaindi"hebu lala huko...usitusumbue!" Mmmh...nikaona hili balaa! Yaan mtu huyu hapa halafu wanasema hawamuoni! Itakuwaje?! Ikabidi nitulie tu...akapiga raundi ya tatu halafu akaja usawa wangu akiwa ukutani akasimama! Nikabaki nashangaa, kitanda kimegota hadi ukutani, huyu anawezaje kutembea bila shida?! Wakati najiuliza nikashangaa kuona ananisogezea mkono wake!! Akisogeza, na mimi nasogea kimyakimya... hadi nikafikia kwenye ukingo wa kitanda, yaani kinachofuata ni kudondoka!! Ujasiri ukanishinda, ikabidi nipige yowee...""baba mtuuuuu!!!" Hapo niko chini tayari!! Sista na mwenzie walivyoskia hivyo ikawa vurugu mechi, na lile giza. Ilikuwa ni mwendo wa kuparamiana tu!!!Dingilai alikurupuka geto kwake na taulo huku kashika panga huku bimkubwa akiwa nyuma yake! Kufika pale kuwasha chemli, akapekuwa hadi uvunguni. Wakaambulia chenga tu, nikawasimulia ilivyokuwa. Ingawa sista nae alidai walivyokurupuka walimuona kabla hajatoeka ingawa simuamini sana. Tangu siku hiyo wote tukawa tunalala chumba kimoja. Na yule binti akakataa kuja kulala. Wiki hiyo hiyo tukarudishwa kwa bibi, dingi akarudi hostel za chuo.

Na kisa kingine nilikutana nacho mwaka ya 2008, ingawa hakikunilenga mimi ila kiliashiria ulozi moja kwa moja. Mimi huwa nilikuwa na tabia ya kupenda kurudi usiku sana nyumbani. Utakuta nakaa home kuanzia asubuh, nafanya shughuli zote. Ila ikifika saa 10 jioni, ndio natoka. Na kurudi ni kuanzia saa 3 hadi 6. Sasa siku hiyo narudi zangu, mida ya saa 4 usiku. Njia ya mkato ina makaburi, naogopa. Njia ndefu kuna kakichaka karefu, kanatisha! Ila huwa napita bila shida. Ila siku hiyo nikajikuta tu naingiwa hofu! Ikabidi nipige moyo konde, maana lazima nirudi home. Basi nikatembea kwa kasi balaa, nikapanga nikikaribia karibu na hicho kichaka nipite kwa kasi ya upepo!! Basi nakaendaaa, nilipokaribia kichaka nywele na mwili vyote vikasisimka. Nikasema leo kazi ipo, nikajikoki...nikatoka nduki la hatari na nakimbia(huwa napenda). Kufika katika ya hicho kichaka nikakuta bonge la kinu limefunikwa!! Hiyo breki na kona niliyokata, Mungu tu ndiyo anajua. Na kipindi hicho nilikuwa niko vizuri kwa mazoezi. Sikugeuka nyuma hadi nyumbani. Niliwaza sana, karibu wiki nzima. Hizi ningekigonga na kubinuka ingekuwaje?! Baada ya mwezi nilimsimulia bimkubwa, alinisema sana! Nikapunguza kutembea usiku. Saa mbili niko home.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 99

    




Sikuwahi shuhudia live uchawi ila niliwahi shuhudia matukio mengi ya kichawi...



Miaka 2007 hadi 9 niliinshi nyumba moja magomeni mikumi karibu na bondeni kule kwa mzee mmoja wanamuita Fungo,



Nikiamka usiku wa manane naenda kukojoa naskia ngoma inachezwa sebuleni kwao waliishi nyumba kubwa mimi chumba cha nje na hiyo ilikua mara nyingi sana kuskia hata ikitokea nikishtuka usingizini naskia wakiimba, kupiga ngoma na kucheza.



Siku nkapanga safari kwenda kusalimia kijijini ikabidi nikubaliane na mzee alale chumbani kwangu maana kulikua na wezi sana miaka hiyo,



Baada ya wiki kurudi nkakuta kapeti limechanwa chanwa sanaaaaa na ni maeneo yale yanayokanyagwa tu, na vipande vimejazana huko chini kibao,

Hata sikuuliza kwa mazingira niliyoyaona nkajua tu ngoma ilihamia gheto kwangu na watakua wanavaa viatu vyenye ncha kali ndio maana wakalichana vile..



Lakini cha ajabu matukio yote hayo sikuwahi kua na hofu hata chembe hata sijui kwanini...



Kuna nyumba tulipanga maeneo ya sinza mapambano, mara nyingi tu mke wangu huona watu wako uchi aidha nje wakichungilia dirishani na wengine wapo chumbani kwetu, na hapo yule macho live, lakini hata anaponiadidhia wala sipati hofu yoyote, hua naona kawaida tu, sijui ni kwanini.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 98

    





Jirani yangu kuna siku alikuwa ananisimulia alikuwa anasafiri na broo wake usiku walikuwa kwenye gari yao. Safari ilivyokuwa inachanganya mbele wakamuona mtu kwa mbali kama anasimamisha gari. Kumuangalia vizuri kumbe ni mwanamke, halafu ni mrembo tu! Dogo akamwambia bro huyu mwanamke atakuwa jini tu haiwezekani usiku huu wote asimame njiani peke yake, tumpite tu.



Brother yake akamwambia usihofu. Akasimamisha gari. Akamwambie ndio mrembo! Yule mwanamke akamwambia naombeni lift nimekwama huu usiku naelekea eneo fulani. Brother yake akamwambia yule mwanamke ingia. Safari inachanja mbuga brother yake akaanza kumwambia yule mwanamke. Inakuaje unatusumbua unasimamisha gari wakati eneo unalotaka kwenda unaouwezo wa kufika?



Yule mwanamke akajibu sielewi unachozungumza. Brother yake akamwambia yule mwanamke, usi' panic! Sisi tuliokupa lift tunajua kwamba wewe ni jini! Ndiyo tunakuuliza kwa nini umetusumbua kusimamisha gari wakati kufika eneo unalotaka uwezo huo unao wewe kama wewe?



Yule mwanamke akawaambia simamisheni gari! Majamaa wakasimamisha. Wakasikia mlango wa siti ya nyuma unafunguliwa. Kugeuka yule mwanamke hawamuoni tena! Brother yake akasema, unatusumbua wakati uwezo wa kufika unao. Wakaendelea na safari.



Nikamuuliza sa mbona huyo jini katumia style ya zamani sana? Jamaa akanijibu, majini ni wapumbavu wapumbavu tu.






USHUHUDA WA KWELI NAMBA 97

    



Kunasiku tulikuwa kwenye mizunguko ya kujioatia riziki Basi tulikuwa wawili kwenye gari yule mwenzangu Yan boss n mwislam ilkua n saa kumi Ile jion n mtu wa dini ikabid aingie kupiga Sala ilkua nakumbuka n charambe Kuna msikiti Kama unatoka mbande unaelea mbagala upo mkono wa kulia na Kama unatoka mbagala to mbande upo mkono wa kushoto Sasa baada ya jamaa kumaliza Sala akarud kwenye gari kuwasha na kuitoa Nissan hard body single cabin pale ikawa mziki ngoma aiendi tukajiuliza inakuaji kushuku angalia Kama Kuna jiwe au nn kinazuia hamna jamaa kaweka reverse hamna mbele hamna kitu tukajiuliza hii n nn hii Basi akaja mzee mmoja hv akaenda mbele ya tair ya mbele chin akachora nakumbuka kitu Kama x kwa fair zote mbili akatuambia nenden aisee kutupia gia mzee gari hyo imeenda tulitoka hapo tukawa tuñacheka tuu kwa kilichotokea Inaonekana pale msikin wale wazee wanaokaaga pale nje n noma sana






USHUHUDA WA KWELI NAMBA 96

    




 Tanga miaka ya 82. Kuna jama alifanya mapenzi na mke wa mtu. Ghafla alipomaliza kitu kikakatikia ndani lkn damu haimwagiki. Alikuja kwa mganga pale Gatundu. Mtu mwingine ukimuangalia mashine unaiona imetulia. Yeye binafsi haioni na hata akipeleka mkono anakuta hamna kitu.

...........,..................



Jamaa mwingine tena alitembea na mke wa mtu. Wakamaliza fresh kila mtu akachukua hamsini zake. Jamaa alikua anakakaa nyumba isiyo na ceiling board. Ghafla wakati amepumzika chumbani kwake ametulia kitandani baada ya kumshuhhulikia mke wa bwege akaona panya amebeba dhakari na pum*** anakatiza nayo kwenye mbao juu





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 95

    




 Vibwengo nishawahi kutana navyo nikitoka bar night kali yaani vifupi kwa mbali vikija unaona kama taa inakufuata vinawaka taa kwenye paji la uso halafu vifupi na vidole vya miguu ya mbele vimegeuka nyuma yaan namaanisha mguu na vidole vinaangalia nyuma kwa hyo vikitembea kwa mbele unaona visogo vya miguu



.ukitembea ukikutana navyo usigeuke nyuma sasa we jitie van dame geuka uone umenikumbusha mbali mzee




USHUHUDA WA KWELI NAMBA 94

    




 Nina chapter mbili (2), moja ya kwangu ma ya pili ni ya baba yangu,

Nitaanza na yangu mwenyewe..

Mwaka 2016 nikiwa na umri wa kati tu usio na tija kuwa mme wa mtu, ila kutokana na misukumo na vishawishi vya barehe ikanibidi nivute kibinti cha kiislam, kutokana na kuwa nilikuwa mpambanaji wazazi wake waliniamini na kunipa mtoto wao japo sikuwa na kigezo hata cha kuoa wakati ule (20+ yrs only) sasa basi baada kufanya process zote ilibidi niowe kiislam kutokana na kuwa waslam hawana mambo mengi(mimi sio muislam wala sina mpango wa kuwa), yaani wao hata mkiwa watu 10 ndoa inatamadadi na kukwishineyi...sasa wakati ule wa binti kuvundikwa baadhi ya wenyeji, dungu&jamaa walianza kumletea zawadi za hapa na pale, baadae ndoa ilifungwa na maisha ya ndoa yakaanza rasmi, sasa kimbembe kilianza baada ya yeye kutoka kwao tu, yaani binti yule akawa mgumu kutoa papuchi ilihali alinipenda mwanzo na alilia ndoa kwa udi na uvumba sasa nikawa najiuliza huyu vipi, ama ananiectia..basi kwa akili zangu za ujana ujana nikawa na-force game, kisha kibishi namaliza ila alikuwa analia sana kana kwamba alifosiwa kuolewa..

Baada ya zile siku saba za mwanzo baada ya ndoa (honey moon) huko kijijini kwetu, tukawa tumejisogeza maghetto kwangu ili tuyaanze maisha yetu wenyewe, sasa hapo ndipo picha lilianza yaani binti kuanzia asubuhi-saa12 mzima kabisa yaani yupo shwari kimbembe ni ile kigiza cha usoni kikianza kuingia yaani alikuwa mwehu kabisa, sasa nikaanza kujiuliza hii imekaaje ama ndio mke ana act ili asitoe mchezo, basi ikabidi nitoe taarifa ukweni maana hali ifikia pabaya sana,

Sasa wakawa wameniambia kuwa jambo hili linavinasaba vya kishirikina, kwa upande wangu sikuamini hata kidogo, sasa bibi wa mke wangu mzaa mama mkwe alikuwa ni mrokole kindakindaki, basi wakawa wame- organize mama&bibi ili mtoto wao atibiwe hayo maswaibu..basi bana siku hiyo nakumbuka niko zangu ghetto sina hamu hata kidogo na ile ndoa si mama mtu akaja na yule Bibi akiwa na wenzake na mama zake wadogo, mama mkwe na wadogo zake ilibidi wabaki nje kutokana na kulinda itifaki ya kutoingia chumba cha mkwilima wake,

Wakawa wametutaka siye wanandoa tupige magoti ili ombi lianze humo humo ghetto, mwanzoni me nilikuwa na- take easy tu nahisi kama vile movie za kibongo, lakini baada ya ombi kukolea nikamuona wife kaanza kupiga mwano, wakabidi wakomae nae me nipo nacheck tu (ilibidi nifumbue macho) ombi likawa ombi daaah mara mtu chini wapo nae tu, mara wakaanza kuyahoji majini baada ya yule binti kuanza kusema mtuache, mnatuchoma..sasa hapo me siamini tu baada ya kuzungumza nayo yakawa yamesema kuwa pindi binti yule anafundwa ndani siku zile za kuvumdikwa kuna mtu alimpea under wear (chupi) kupitia kwa mdogo wake, yeye pasina kujali akawa kaivaa, na ndipo yalianza maswaibu..me bado hapo sina imani tu na kile kinachoendelea, baadae kabisa baada ya ombi kukolea yule binti akaanza kutema nyama nyama kama stake hivi ila zipo mithiri ya damu iliyoganda, wakachukua mtandio wake wakaanza kumtoa zile nyama mdomoni pia alikuwa anatafuna meno kiasi kwamba unasisimuka kama mtu anae sugua sifuria, hapo sasa ndio nikaanza kupata imani kuwa kweli binti yule ana jambo tena kubwa tu, baada ya ombi kumchek yule binti mdomoni nilishangaa hakuwa na jeraha wala kovu ambalo lilisababisha kutoa nyama zile tena zimejaa kwenye mtandio wake wa kiislam..mzee nilidata mpaka nikakoma na kimbelembele changu cha kuyakimbilia mapenzi,

Baada ya ombi lile tukawa kama temeyaamsha, na siku zilizofuata ndio kikawa kimbembe zaidi ya mwanzo, maana kuna usemi unadai kuwa kama wewe umeombewa na kutokwa na majini basi unatakiwa uishike imani sana sana laasivyo huwa yakitoka 10 yanarudi 20 it means (2x2), sasa sisi tuka- take easy kabisa, yaani majanga yalizidi mpaka kufikia hatua ndoa kuota mbawa ndani ya mwezi mmoja tu(mpaka sasa nipo single, na sina hamu kabisa ya kuwa na mke).

Yaani yule binti alipoteaga, wazazi wake waliuza nyumba ili kumtafuta binti yao kwa wataalamu, walimpata baadaya ya mwaka mmoja (2017) ila waliyumba sana kiuchumi na kuhama mji waliokuwa wanaishi na kwenda kwingine kuanzisha maisha tena ya upangaji, baba mkwe wangu na baba yake mzazi mpaka leo hawasemshani maana ktk jopo lililohusika na hizo inshu pia mke mdogo wa huyu babu wa mke wangu alihusika sana, pia huyu babu hakuwahi kusimama kumtetea mjukuu wake wakati wote alisema kuwa mkewe anasingiziwa huenda ni kutokana na limbwata ama juju alilopewa na huyo mke wake



NB: pia kipindi tunamuuguza mke wangu tuliwahi kwenda kutibiwa kwa mmoja wa bibi zake wa ukoo tukiwa huko, me nyege zikanizidi ikabidi nimuombe show wife maana tulilala kitanda kimoja, alivyogoma kutoa mechi ikabidi nitumie force maana nilikuwa na kama wiki kadhaa pasipo kufanya chochote kwake na isitoshe kwa wakati huu alikuwa keshapona(hapandwi na majini wala hakuwa kichaa), yule bibi alituachia room ambayo ilikuwa ndio kilinge chake, Aiseee nakumbuka wakati na-force kuchojoa chupi nae hayumo kelele zikawa kibao wakati huo ni kama saa11 alfajiri, mara paaap nasikia sauti kwenye angle ya kuta ikisema shiiiiiiiiii, daah nilitoka nje nikiwa na boxer yangu tu hapo nipo kifua wazi nikamfuata yule bibi akaniambia nitulie tu nikiwa ndani maana kilingeni huwa hakuhitaji makelele, sikuomba match tena wala sikusinzia mpaka kunapambazuka kisha nikasepa zangu kurudi mjini..





BLOG