Search This Blog

Thursday, November 3, 2022

USHUHUDA WA KWELI NAMBA 120

    




Mwaka 2002 nikiwa bado yanki wa chekechea tu nina miaka yangu saba nilikuwa na katabia kamoja matata sana. Wazee wangu wanapotoka then wananiambia nibaki nilikuwa nakubali then nawafuatilia nyuma wakifika mbali sana najitokeza kwa vile ni mbali wanakosa jinsi inabidi twende wote tu. Tulikuwa tunaishi ubungo msewe kwa chini kidogo,kwenye lile ghorofa la Tanesco lililovunjwa,ukivuka barabara na kuteremkia bondeni,unavuka mto kisha ukupandisha unakutana na uwanja wa mpira,kushoto mwa uwanja kuna makaburi na katikati ya makaburi kuna njia ndogo ya mkato.



Mandhari ya eneo la makabuli,kulia kuna nyumba mbili ama tatu hivi zimejengwa kuzunguka makaburi,kuna vichaka vya maua na miti ya vivuli,kushoto kuna nyumba moja kubwa ya kifahari,miti ya maua na vivuli inakutana katikati ya njia,njia hii ina ukubwa wa hatua mbili hivi za mtu mzima,kingo zake zimepandwa maua,njia inayagawa makaburi katika sehemu mbili zilizo sawia.





Miti hii kwa juu imeshonana kiasi na kufanya njia iwe mfano wa barabara zinazotobolewa katikati ya mwamba au mlima(Tunel)sehemu ya kuingilia imepambwa kwa maua na kuwa kama mlango wa pango hivi sawia na upande wa pili wa kutokea eneo hili(ilichagizwa na maua yanayotambaa kama mapesheni siyajua jina lake maua yametambaa juu ya miti) Basi hiyo siku nimeona wazazi wangu wanajiandaa kutoka kwenda kwenye harusi ,Mikocheni na sijataarifiwa na mimi nijiandae,nikaelewa! Nikachukua nguo nzuri(mayanki wa kipindi hiko wanaelewa maana ya nguo nzuri) nikazificha nje pamoja na viatu,nikawangojea watoke na mimi nikatoka,nikavaa chap na kuamza kuwafuata nyuma,huo muda ilikuwa saa mbili usiku kuelekea saa tatu. Nikiwa nimewaacha umbali wa kama hatua kumi hivi,mwendo wa dakika tano tu ulitosha kutufikisha eneo la makaburi,nikasimama na kuwaacha waingie kuvuka nikawahesabia timing kuwa washavuka na mimi ndio nikaanza kuvuka.



Kwa vile nyumba zile tatu hazikuwa mbali sana mwanga wa taa uliangazia kidogo sana eneo hili,nikaanza kupiga hatua,harufu kali ya marashi ambayo hadi leo sijawahi kuyasikia niliyasikia vizuri sana,ile kutupa macho mbele namuona msichana mburushi,sijui mwarabu kasimama tuli pembeni ya njia ananiangalia ninavyozidi kumkaribia. Nywele zake zilikuwa ni nyeusi na ndefu karibia kugusa kiuno,gauni jeusi lenye mng'ao hafifu,midomo ilikuwa na lipstick nyekundu,macho makubwa meupe na alikuwa amefumbata mikono yake kwa kuipishanisha kifuani kama wafanyavyo mabosi wengi wa mjini. Kiroja kikaanzia hapa,kadiri navyomkaribia naye alikuwa anaongezeka urefu,wakati alikuwa mfupi kiasi lakini hadi namfikia ili nimpite tayari asingeweza hata kupita mlangoni labda kwa kuinama kidogo.



Nikamfikia na kumsalimia shikamoo,akaitikia mar habaaaa,wakati huo nimegeuza shingo juu kumtazama naye alinitazama,baada ya kumpita na na kumwacha hatua kama tano hivi,hizo mbio nilizotoka nazo kwakweli sikumbuki kuwahi kuzikimbia mbio kama zile. Nikaliacha eneo la makaburi na kuteremka bondeni,nikavuka kidaraja na kupandisha barabarani,nikawasili kituoni(hiki kituo kwa mbele ndio unatazamana na jengo la Tanesco lililovunjwa,ile kutazama huku na huko wazee siwaoni na watu ni wengi,kiasi kwamba watu wakaamza kuhisi nimepotea wakataka wanishike wanihoji vizuri,nikawaponyoka nikashusha bondeni ili nirudi nyumbani. Hatimaye nikafika eneo la makaburi,nikasimama nikijishauri kupita,moyo wangu uligoma,ulikataa katakata na hapo inaelekea saa nne na nusu usiku,nilichokifanya ni kuzunguka njia ndefu kwelikweli,nilitumia lisaa na nusu kuzunguka wakati kama ningekatiza makaburini ingekuwa safari ya dakika kumi tu!





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 119

    




Haahah,kuna kisa cha mpemba Mafia, alikua ameanika samaki wake baada ya kuwavua, ikafika mda akatoa mkeka akawa anapiga rakaa(Anaswali).Amemaliza kuswali kugeuka hamadi samaki wake wawili hawapo, akauliza kuna ntuu kachukua samaki zangu arudishee kila mtu akakakana akasema mi natoa dakika kumi tuu msiporudisha Walah! atakufa mtuu hapa na si masiharaa... Ebanaeee baaada ya dakika 10 zikaanguka kunguru mbili(hawa ndege Weusi) zimeshakaukaa zamani mdomoni wanamabaki ya samaki....





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 118

    



Na huko kuelekea Lukozi ndio kuna msitu unaitwa 'kandele ka paa' huko ndio kuna mapicha sio ya nchi hii, waulize waendesha magarii...



Na ukitokea huko mkuzi...

kimbembe kipo pale kati ya msitu kwenye daraja flan kubwa, maji yanayopita ni mengi ila yanashuka taratbu, kila upande ni giza kubwa si barabarani sio msituni maana maeneo hayo ndio msitu umefura kisawa sawa na miti ni mikubwa mirefuuu kwaio hata mwanga wa jua haupenyi...



Kwaio pana sifa ya Ukimya, giza kubwa, msitu mnene, Daraja kubwa lenye maji mengi,

You can imagine....



pale Hata walevi wakipita wanaacha kelele kwanza.. ndio utajua Pombe inaogopa nayo..

Maji yenyewe hayapigi kelele wala ndege wa polini wewe upge kelele ni nani?....

Pametokea matukio mengi sanaaa.....



Yote kwa yotee yale maeneo yana mapicha picha sanaaaa...

Huko huko mkuzi kuna mzungu mmoja maarufu sana naamini hata wewe unamfahamu, alikua anaitwa mzuka,



Kisa cha kupewa hili jina ni kwamba alikua na shamba akaambiwa popote utakapoona huu mti usiukate ni makazi ya majini/shetani..

Akapuuza siku akaukata...

Alikula bonge ya banzi, kuanzia pale akawa amepinda shingo, kichwa kimelalia upande mmoja...



Maisha yake yote yaliobaki alikua akitembea na kikapu kilichojaa mawe upande mmoja ili ku balance mwili maana ulikua umelala upande mmoja...



Pia tushawahi pita sehemu usiku miti ikalala yoteee.....

Pia mzee alishawahi salimiwa na vibwengo usiku akitoka magamba coast akipita ule uchocholo wa magamba sec...

Akavitukana sana huku anachomoka kasi ya ajabuu..

alifika nyumbn hana kiatu kimoja.....



Kuna mapicha mengi sanaa kulee....

Yale maeneo yote yalikua makazi ya wajerumanii,

nyumba nyingi km ya mkapa, ngwirizi na majumba mengi sana yamejaa...



Hata sisi kambi yetu ilijengwa na mjerumanii,

Majumba yao yamedizainiwa kiajabu sanaa....

Tumeish kwenye nyumba miaka na miakaaa,

eti tunakaribia kuhama ndio tunajua tunaishi juu..

kumbe chini kuna nyumb nyingne yenye mavyumba na hapo barazani chini kumbe ni bonge ya kisima..



Ilikua ukizunguka msituni kukuta sehemu imesakafiwa au makorokocho korokocho mengi ni kitu cha kawaidaaa..



Nimepamisss long time sanaaaa..





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 117

    




Alikuwepo mfanya biashara mmoja huko(alikuwa anafanya biashara za magendo) basi kila alipokuwa anapita na pikipiki yake akawa anasumbuliwa na askari mmoja wa barabarani ikabidi awe anatoa hongo ili asikamatwe ilifika time akachoka kutoa hongo.



Siku mmoja akapita kama kawa akasimamishwa na yuleyule askari. Alikuwa na ndoo amefunga kwenye pikipiki yule askari akaenda kukagua haaa akakutana na kichwa cha mtu kinatoa damu mbichi kana kwamba kimekatwa muda huohuo.



Askari aliruka kwa mshtuko maana hakutarajia kuona kitu kama hicho wenzake kufika pale kwenye ndoo hawaoni kitu.



Unaambiwa alitoka pale moja kwa moja kuomba uhamisho kurudi kwao.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 116

    




Mwaka fulani nikiwa katika mafunzo ya JKT katika kambi moja wapo hapo Kigoma,

Kuna ServiceMan mwenzetu alimua kapangiwa lindo huko ndichi mashamani, mchana akiwa lindoni akakutana na bibi kabeba mkungu wa ndizi za jeshi, Basi Service akachukua ndizi na bibi akarushwa sana kichura, mwendo wa bata na kupiga push za kutosha kisha akaachiwa andoke zake.



Jioni jamaa anarudi Hangani(Dom) baada ya kukabidhi silaha akaanza kuumwa sana mpaka asubu ni mahututi, hospitali wanadai hawaoni ugonjwa basi Nyumbani kwao wakamuomba akaenda kutibiwa na akapona, Siku anarudi kambini ile hali inaanza upya, akitoka nje ya kambi mzima ila akiingia kambini hoi. Mpaka Utawala wakamumisha Kambi.



Shkmaooo Kigoma.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 115

    





Kama mtaikumbuka ile mvua ya mawe kahama march 2015 ngoja niwape kisa chake.



Mvua zilikuwa adimu sana basi wananzengo wakamfuata mganga mmoja alokuwa ana tuhma za kuzuia mvua

Basi watu wakamuhoji akakataa tuhuma hizo. Jamaa hawajaelewa wakampiga hadi kumuua.

Wakati anakufa alisema nakuta lkn mtaona.

Waloelewa walianza kuhama walokaza shingo wakakomaa .....

Mvua ilipoanza wakasema tumemuua yule alikuwa anazuia mvua....lkn ikaja kuzidi....na mawe juu. Iliua watu na mifugo na uharibifu mkubwa ulotokea.





USHUHUDA WA KWELI NAMBA 114

    





Wale waliosoma boarding mnamkumbuka miss corridor sjui nyie mlimwiitaje in short huyu ni jini huwa anatembea ukumbuni kwenye mabweni mashuleni au makambini au maholi tulitunga hilo jina sababu akitembea unaskia "ko, ko, ko " ile sauti kama ya viatu vya kike vyenye visigini virefu ukienda angalia huoni mtu ukibahatika unamuona mwanamke ana nywele ndefu kakupa mgongo anamalizia kukata kona

 miss corridor,, umenikumbusha mbali sana.. vyooni kulikuwa hakuendeki usiku hata mbebane kumi mkisikia hiyo "ko" au mlango umejibamiza "pa" wote mnatoka nduki kila mtu na hamsini zake,, chumba kilicho karibu yako ndiyo unaingia unajibanza humo humo hamna kuulizana tutajuana asubuhi.. wallahi maisha ya boarding kuna muda yananifanya namiss sana skuli

 





BLOG